Business
Biashara ya Mananasi yakabiliwa na changamoto Kilifi
Wafanyibiashara kuuza matunda aina ya Nanasi kaunti ya Kilifi wanasema biashara ya matunda hayo inazidi kudorora msimu huu ikilinganishwa na msimu uliopita.
Kulingana na wafanyibiashara hao, matunda ya Mananasi hayapatikana kwa urahisi sokoni kutokana na mabadiliko ya hali ya angani licha ya biashara ya matunda hayo kuwa na thamani kubwa katika soko la Pwani na taifa.
Wakiongozwa na Japhet Khambi, wafanyibiashara hao walisema kwa sasa wanategemea matunda hayo kutoka nje ya nchi hasa taifa la Uganda ambapo uagizaji wa matunda hayo umekuwa ghali mno.
Katika suala la usafirishaji wa bidhaa hiyo katika soko la kaunti ya Kilifi kutoka taifa hilo jirani la Afrika Mashariki, wafanyibiashara hao walisema ghamara ya usafiri uko juu mno hali ilichangia bei ya bidhaa hizo kuongezeka mara dufu.
“Hii mambo ya gharama ya usafirishaji na uhaba wa matunda hayo bei ya bidhaa hiyo imepanda kwa kiwango kikubwa, alieleza Khambi.
Wafanyibiashara wa matunda ya Mananasi walisema Nanasi ambalo lilikuwa Linanunuliwa kwa shilingi 100 sasa tunda hilo limepanda bei na kuuzwa kwa shilingi 250.
“ Tulikuwa tunanunua Mananasi kutoka eneo la Chakama katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi kwa bei nafuu lakini kwa sasa hayapatikani na kutulazimu kuangiza matunda kutoka Uganda.”, alisema Khambi.
Taarifa ya Pauline Mwango