Sports

Stars Yapiga Sare Na Chad

Published

on

Timu ya taifa Harambee Stars imekabwa koo sare tasa na taifa la Chad mechi ya Kirafiki ugani Stade De Marrekech Jumamosi.

Vijana wa kocha Benni McCarthy walikosa Fursa Chungu nzima ya kufunga katika mechi hiyo huku kocha Benni akianza na washambulizi Williamson Lenkupae na Adam Wilson ambao wote wanacheza Ugaibuni.

Matokeo hayo yanamanisha kocha huyo mpya sasa ameongoza vijana hao mechi tatu bila kushinda tangu achukuwe usukani kuongoza timu ya taifa kwani mechi ya kwanza alitoka sare magoli 3-3 na Gambia,kabila ya kupoteza magoli 2-1 dhidi ya Gabon.

vijana wa nyumbani wanaingia uwanjani tena siku ya jumanne huku kocha McCarthy akisaka ushindi wa kwanza kama mkufunzi wa Stars.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version