News

Wakaazi wa Mariani eneo la Adu walalamikia ukosefu wa maji

Published

on

Wakaazi wa eneo la Mariani wadi ya Adu eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi wanaitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kukamilisha mradi wa maji ulioanzishwa eneo hilo ili kuwawezesha kupata huduma za maji kwa urahisi.

Wakaazi hao, walidai kwamba tangu tenki la mradi huo wa maji kuwekwa eneo hilo miaka 3 iliyopita, bado limesalia bila maji hali inayozidi kupoteza matumaini yao ya kusaidika kupitia mradi huo.

Wakaazi hao walielezea kupitia masaibu mengi hasa wakati wanapotafuta maji kwani hulazimika kutembea mwendo mrefu ili kupata bidhaa hiyo muhimu.

“Tulianzishiwa mradi wa maji ili kujiendeleza kimaisha kutokana na shida tuliyokuwa nayo miaka mingi lakini hadi sasa hakuna msaada wowote tuliyopata kwani tenki la maji lililowekwa hali maji miaka mitatu sasa”, alisema mmoja wa wakaazi hao.

Haya yanajiri huku maeneo mbalimbali ya Magarini yakiendelea kushuhudia uhaba mkubwa wa maji hasa baada ya kuanzishwa kwa miradi ya maji na kisha kukwama.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

1 Comment

  1. Janet

    August 21, 2025 at 5:58 pm

    It’s true

Leave a Reply

Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version