News

Achani: Kaunti ya Kwale imepiga hatua katika uchumi samawati.

Published

on

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amesema kaunti ya Kwale imepiga hatua katika kuimarisha sekta ya uvuvi na uchumi samawati.

Gavana Achani ameihimiza serikali ya kitaifa kuhakikisha inawekeza zaidi katika masuala ya uchumi samawati hasa kupitia bandari ya Shimoni, akisema itafungua ajira kwa vijana na kuboresha uchumi wa kaunti.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya sherehe za 62 za Madaraka katika eneo la Kinango, Gavana Achani amesema bandari ndogo 9 katika kaunti hiyo zimeboreshwa na vifaa vya kisasa ili kuchangia uhifadhi wa samaki.

Maadhimisho ya sherehe za Madaraka eneo la Kinango

Hata hivyo Viongozi waliohudhuria sherehe hizo katika gatuzi dogo la Kinango wakiongozwa na Mbunge wa Kinango Gonzi Rai, wamesisitiza haja ya viongozi pamoja na wananchi kumuunga mkono Rais Ruto katika kufanikisha ajenda ya maendeleo.

Kwa upande wake Kamishna wa kaunti hiyo Stephen Orinde amesisitiza umuhimu wa wakenya kuunga mkono miradi ya serikali hasa uchumi samawati na masuala ya bahari ili kupiga hatua kimaendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version