Sports
Amani Kupitia Michezo Kati Ya Polisi Na GenZ
Baraza la Makanisa Nchini IRCK kwa ushirkiano na Kilifi Inter Faith Network pamoja na Wizara ya Usalama wa Ndaani imeenda mechi ya soka ya Amani kati ya Maafisa wa Polisi na vijana wa Kilifi Kaskazini ugani Karisa Maitha hii leo.
Katika mechi hiyo ya kirafiki vijana wa Kilifi GenZ wameibukia na ushindi wa magoli 4-0 mechi ulioshuhudia ushindani kutoka kwa timu zote mbili.
Akizungumza kwenye hafla hiyo mgeni Mweshimwa OCPD Kilifi Stanley Tonui ametaka vijana kuhubiri Amani na kujua polisi na wao ni marafiki na mandugu wanaohitaji ushirikiano kufanikisha shughuli zao za kila siku.
“Kwanza kabisaa Nishukuru waandalizi wa mchezo huu wa leo,ni hatua mazuri ili kujenga nchi iliobora,Nchi ya Kenya haiwezi iakendelea bila walinda Usalama kwa hiyo sote tunahitajiana.”
Kauli yake ikiungwa mkono na afisa wa mipango katika Baraza la Makanisa Nchini Anthony Blaiz ambaye amesema kwamba njia ya pekee ya Tujenge trust ni kupitia michezo.
“Tunajenga uhusiano mwema kupitia michezo kwani ndio njia pekee kama ilivyo kwenye jezi zetu ,We Build Trust Through Play,muhimu Sanaa ni Amani.”
Naye Askofu mkuu na Mwenyekiti wa kilifi interfaith network amos lewa akisema michezo ni silaha ya amani kwa vijana akiongezea ni heri tutoe jasho tukijenga Amani na sio kutoa damu wakati wa vita.
“Ni Heri tutoe jasho tukijenga Amani kuliko tutoe damu Wakati wa Vita.”
Malengo ya mchuano huo ulikua ni kuhubiri Amani nchini kati ya Polisi wa Taifa hili na GenZ.