News

Askofu Kivuva atoa wito kwa serikali kusuluhisha mgomo wa Wahadhiri

Published

on

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mombasa Martin Kivuva ametoa wito kwa serikali pamoja na Wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma nchini kuanzisha mazungumzo ya haraka ili kutatua mgomo wa wahdhiri unaoendelea kote nchini.

Askofu Kivuva alisema mgomo huo ambao sasa umeingia siku ya 11, umeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za masomo katika vyuo vikuu vya umma nchini.

Kivuva alisema hali hiyo ikiendelea huenda ikaleta madhara makubwa kwa elimu ya juu na mstakabali wa wanafunzi huku akisisitiza kwamba suluhu la kudumu linaweza kupatikana kupitia mazungumzo ya wazi kati ya pande zote mbili.

“Mgomo sharti uishie watu kuzungumza na kuweka mikakati, siku zote bila maridhiano ama kuridhika moyoni ni vigumu sana watu kusonga mbele, jambo hilo la Wahadhiri kugoma pia ni changamoto inayokumba nyanja ya elimu”, alisema Askofu Kivuva.

Wakati huo huo aliisihi serikali kutimiza ahadi ilizotoa kwa Wahadhiri, ikiwemo kuwalipa mishahara na marupurupu yao, akisisitiza kwamba haki za wafanyakazi ni lazima ziheshimiwe ili kuhakikisha utulivu katika sekta ya elimu.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version