News

Bodi ya Hazina ya fedha ya Mombasa yaapishwa

Published

on

Serikali ya kaunti ya Mombasa imeapisha rasmi bodi ya kwanza ya hazina ya fedha ya Mombasa, hatua inayoweka msingi wa utekelezaji wa sheria ya hazina hiyo ya mwaka wa 2026.

Hazina hiyo inalenga kutoa mikopo nafuu kwa wajasiriamali, vijana, wanawake, vyama vya ushirika, biashara ndogondogo kupitia mafunzo, uongozi bora na usimamizi wa fedha.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharif Nassir alisema bodi hiyo itaanza mara moja kuandaa mifumo ya utekelezaji ili kuhakikisha wafanyabiashara wanapata huduma za kifedha kwa wakati, hatua itakayochochea kuwepo na nafasi za ajira, kupanua fursa za kiuchumi na kuimarisha uchumi wa Mombasa.

Bodi hiyo itaongozwa na mwenyekiti Samuel Omondi Okech, huku Munira Hamisi akiwa Afisa Mkuu Mtendaji.

Bodi ya hazina ya fedha ya Mombasa kaunti ya Mombasa imeapishwa rasmi, chini ya uangalizi wa Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir

Wengine ni Elizabeth Sonia Michael, mwakilishi wa wanawake, Abduswamad Noor mwakilishi wa watu wenye uatilifu, Hamza Kombo mwakilishi wa vijana, Hamisi Kurichwa afisa Mkuu wa biashara na Swaleh Mwalizuma, afisa mkuu wa fedha na mipango ya uchumi.

Kuapishwa kwa bodi hiyo kunatajwa kuwa hatua muhimu katika juhudi za Serikali ya Kaunti ya Mombasa za kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika ukuaji wa uchumi na kunufaika na maendeleo ya kaunti.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version