News

Chanjo elfu 5 za Mpox zawasilishwa Mombasa

Published

on

Serikali ya kaunti ya Mombasa imethibitisha kupokea jumla ya chanjo elfu 5 za homa ya Mpox kutoka kwa wizara ya afya nchini.

Chanjo hizo zinalenga kutolewa kwa watu walio katika hatari kubwa ya maambukizi, hasa madereva wa malori wa masafa marefu na wakaazi wa maeneo yaliyoathirika zaidi hasa maeneo bunge ya Jomvu na Changamwe.

Zoezi la utoaji wa chanjo hiyo linatarajiwa kuanza kati ya tarehe 3 hadi 12 Septemba mwaka huu, likilenga kupunguza kasi ya maambukizi katika maeneo yalio na visa vingi vya Mpox.

Wakati huo huo, Kaunti ya Mombasa imeanzisha kampeni ya kutoa hamasa kwa wahudumu wa afya kuhusu zoezi hilo ili kuhakikisha ufanisi katika utoaji wa chanjo.

Kulingana na takwimu kutoka Wizara ya Afya nchini, kaunti ya Mombasa inaongoza nchini kwa idadi ya maambukizi ya homa ya Mpox, ikiwa na jumla ya visa 178 vilivyoripotiwa.

Taarifa ya Mwanahabari wetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version