Sports
Chelsea Kumtambulisha Delap
Mshambulizi wa kilabu ya Ipswich Town na timu ya taifa Uingereza Liam Delap amekamilisha sehemu ya kwanza ya vipimo vya kimatibu anapokamilisha uhamisho wake katika kilabu ya Chelsea.
Kwa mujibu wa gwiji wa uhamisho barani ulaya Fabrizio Romano uhamisho huo ni wa pauni milioni 30 Delap akitarajiwa kumwaga wino mkataba wa miaka mitano stamford bridge.
Licha ya kumulikwa na vilabu kadha wa kadha ikiwepo Manchester United pamoja na Newcastle United Delap aliamua kwamba chaguo lake ni Chelsea msimu huu na atakua sajili wa kwanza kwa kocha Enzo Maresca.
The Blues wanatarajiwa kumtambulisha hii leo mchezaji huyo ambaye alipachika wavuni magoli 12 msimu huu na kutoa pasi mbili kwa wenzake kufunga msimu ambao umekamilika.
Vijana hao wanaaminika pia kusaka mshambulizi tajika msimu huu wakimulika mshambulizi Victor Gyokeres na Victor Osimhen inaamnika pia wanamfukuzia winga wa Bilbao Nico Williams.