News
Christine, ahimiza umuhimu wa kutunza mazingira
Naibu gavana wa kaunti ya Taita Taveta Christine Kilalo amewataka wenyeji kuimarisha mazingira kwa kudhibiti utupaji wa taka kiholela hasa katika maeneo ya Taveta na Voi.
Kilalo alisema taka hizo za plastiki zimekuwa zikichafua mazingira hali ambayo inampa msukumo wa kuitaka jamii kuwa katika mstari wa mbele katika kuziokota.
Aidha, Kilalo alisema watahakikisha kuwa suala la uzoaji taka katika miji mikuu ya kaunti hiyo linapewa lipaumbele.
Vilevile, Kilalo alisisitiza umuhimu wa wenyeji kushirikiana na serikali ya kaunti hiyo ili kuhakikisha mazingira yameimarishwa.
“Lakini mwaka huu tuzingatia masuala ya kumaliza kabisa utupaji wa plastiki katika mazingira yetu’’ alisema Kilalo.
Taarifa ya Janet Mumbi