News

Daktari Johansen: Uchunguzi wa miili 34 Kwa Binzaro umebaini watu hao waliuawa

Published

on

Uchunguzi wa miili iliyofukuliwa kutoka kwa makaburi kwenye kijiji cha Kwa Binzaro kaunti ya Kilifi umeonyesha kwamba baadhi ya miili hiyo ni ya watu waliouawa kimakusudi kwa kupigwa na vifaa butu au kunyongwa, jambo ambalo limezua tetesi ya vitu vya lazima.

Kundi la maafisa wa Uchunguzi wa maiti na wataalamu wengine wakiongozwa na mkaguzi mkuu wa maiti wa serikali Daktari Johansen Oduor, kufikia sasa tayari limechunguza miili 34 iliyofukuliwa au kupatikana katika msitu wa kijiji cha Kwa Binzaro.

Maafisa hao waliweka wazi kwamba kuna kila dalili huenda watu hao waliuawa na sio kupitia kufunga hadi kufa kwa mujibu wa imani za kiitikadi.

Uchunguzi huu sasa unzua maswali mengi kuhusu sakata ya Shakahola.

Mapema wiki hii, Watu wanne walifikishwa Mahakamani mjini Malindi wakikabikiwa na kesi ya mauaji ya halaiki ya watu katika kijiji cha Kwa Binzaro.

Hakimu mkuu wa Mahakama ya Malindi Joy Shiundu Wesonga, aliagiza kuendelea kuzuiliwa korokoroni kwa wanne hao kwa siku 60 zaidi hadi kesi yao itakaposikizwa tena mnamo tarehe 2, Oktoba mwaka huu.

Wakati huo huo kitengo cha ufukuzi wa miili tayari kimetambua makaburi zaidi ya wafu yanayoaminika kuzikwa waumini wa dini hiyo potofu.

Washukiwa hao ni pamoja na Kahindi Gharama, Thomas Mukonwe, James Kahindi Kazungu na Sharleen Tembo Anindo wanaohusishwa na mashtaka ya kuendeleza mafunzo ya dini potofu, ugaidi, itikadi kali na uhalifu uliyosababisha baadhi ya waumini kufunga hadi kufariki.

Taarifa ya Eric Ponda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version