News
EACC yafaulu kurejesha shilingi bilioni 7.8 zilizoporwa.
Tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC imesema imefaulu kurejesha shilingi bilioni 7.8 zilizoporwa.
EACC kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari, imeeleza kwamba fedha hizo zinajumuisha mali na raslimali za umma zilizopowa na baadhi ya wakenya wasiojali maslahi ya wengine na maendeleo ya taifa.
Tume hiyo ambayo ilitikwa jukumu la kukabili ufisadi na kuendeleza uadilifu kwa maafisa wa umma, mashirika na taasisi imekuwa ikifuatilia sakata mbalimbali za ubadhirifu wa mali ya umma ambao mara nyingi umekuw ukitekelezwa na baadhi ya wakenya ikiwemo viongozi wa kisiasa na maafisa wa idara mbalimbali za kiserikali.
Tume hiyo ya EACC ilifafanua kwamba kumekuwa na ongezeko la visa vya uporaji wa mali ya umma, ikisisitiza kwamba maafisa wa Tume hiyo wako makini kuhakikisha ufisadi nchini unakomeshwa.
Afisa mkuu mtendaji wa EACC Abdi Ahmed Mohamud, alisema kwamba viwango vya ufisadi nchini vingali juu na makachero wa EACC wamefanikiwa kukabiliana na visa vya ufisadi kwa asilimia 72 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Mohamud aliongeza kuwa tume hiyo imefanikiwa kurejesha shilingi bilioni 7.8 zilizokuwa zimeporwa katika kipindi cha miaka miwili, huku akiahidi kwamba mikakati zaidi imeekezwa kuhakikisha ufisadi unakomeshwa nchini.
“Juhudi tulizoweka katika kukabiliana na ufisadi nchini zimefaulu lakini kuna haja ya ushirikiano na washikadau
Wakati huo huo alieleza wasiwasi wake kuhusu kiwango cha hasara kilichorekodiwa katika miaka ya hivi karibuni akifichua kuwa takriban shilingi bilioni 10.74 zilipotea kupitia ufisadi katika kipindi chab miaka miwili pekee iliyopita.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi