News

Familia ya jamaa aliyezama baharini inalilia haki

Published

on

Familia ya Mwanamme aliyezama baharini katika kaunti ya Kilifi siku kadhaa zilizopita, inahimiza serikali kuongeza juhudi na kuwapa msaada wa kumtafuta jamaa wao.

Ikiongozwa na Omar Ali Omar ambaye ni Kakake Marehemu, Familia hiyo ilisema wamekuwa na wakati mgumu wa kuelekea baharini kila siku kwani kufikia sasa ni siku ya nne tangu jamaa wao azame baharini.

Aidha aliitaka serikali ya kaunti kutoa taarifa sehemu mbalimbali zinazopakana na ufuo wa bahari kwani huenda mwili wa Marehemu ukasukumwa na mawimbi hadi ufuoni. 

Familia ya jamaa aliyezama maji inalilia haki

Omar aliitaka idara ya kukabiliana na majanga katika kaunti kushirikiana na wavuvi wengine eneo la Mnarani pamoja na kutuma maboti zaidi kwa ajili ya uokozi wa mwili wa jamaa huyo kwani wamelazimika kugharamikia mafuta ya boti za ziada.

“Rescu timu ni boti moja, hiyo pekee yake kutafuta mtu kwa bahari ni vigumu vyombo vinatakikana vitoke vingi,washirikiene na sisi familia tuwekuongeza vyombo vya baharini kutafuta jamaa wetu, kwa sasa tunagharimika sasa boti kwenda baharini asubuhi na jioni inatugharimu shilingi elfu 16 kwa siku”, alisema Omar.

Kauli ya Omar imeungwa mkono na Mamake Marehemu ambaye ameshinikiza serikali ya kaunti kuingilia kati na kuhakikisha mwili wa mwanawe unapatikana.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version