News

Familia ya mwendesha bodaboda Watamu yalilia haki

Published

on

Familia ya kijana wa umri wa miaka 22 aliyefariki baada ya kupigwa risasi na polisi imeitaka mamlaka ya kutathmini utendakazi wa maafisa wa polisi IPOA kufanya uchunguzi wa haraka na kuwachukulia hatua polisi waliohusika.

Inaarifiwa kijana huyo aliuawa alipokuwa katika kazi yake aneo la Watamu kaunti ya Kilifi.

Marehemu ametambulika kama Kazungu Jefwa na alipigwa risasi bahati mbaya alipokuwa akiendelea na shughuli zake za kazi ya boda boda katika eneo hilo la Watamu.

Maafisa wa kutetea haki za kibinadam wakiongozwa na Walid Sketty wa shirika la la Vocal Africa walisema kisa hicho kilitokea baada ya vurugu lililohusisha maafisa wa polisi na mshukiwa mmoja wa pikipiki ambaye baadaye aliuliwa na wananchi.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version