News
Francisca atoa wito kwa vijana kuwania nyadhfa za kisiasa
Waziri wa masuala ya kijamii na ukuzaji wa talanta katika serikali ya kaunti ya Kwale, Francisca Kilonzo ametoa changamoto kwa vijana hasa wa Kike kwenye kaunti hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuwania nyadhifa mbalimbali za kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027.
Kilonzo aliwataka kuwania nyadhfa za uongozi wa kaunti ya Kwale sawia na bunge la kaunti hiyo ili kuhakikisha idadi ya wanawake waliochaguliwa inaongezeka.
Kilonzo na Mwakilishi mteule katika bunge la kaunti ya Kwale Judy Kengo walisema ikiwa vijana hao watazingatia hilo kutakuwa na ongezeko la Wanawake serikalini.
‘’Na ni Kwale pekee ambapo unaona viongozi ambao wamechaguliwa ni kidogo ukilinganisha na zile kaunti zingine za maeneo ya kati miongoni mwa zingine viongozi ambapo idadi iko juu’’, alisema Kengo
Naye Afisa wa mipango katika shirika hilo Rachel Akinyi na mmoja wa wanawake katika kaunti hiyo, Furaha Nyuki wameitaka jamii kuwaunga mkono wanawake kwenye uchaguzi huo mkuu ujao.
Taarifa ya Janet Mumbi