News

Furaha Chengo ajiuzulu kutoka chama cha DCP

Published

on

Mgombea wa nafasi ya ubunge wa Magarini kaunti ya Kilifi kwa chama cha Democracy for Citizens Party DCP Furaha Chengo Ngumbao maarufu Kalama Wehu amejiuzulu kutoka chama hicho.

Furaha ambaye ni Wanachama wa Kamati kuu wa kitaifa wa chama hicho, alisema bado yuko kwenye kinyang’anyiro cha ugombea wa ubunge wa Magarini lakini kwa tiketi ya chama kingine.

Katika barau yake kwa makao makuu ya chama hicho, Furaha alitoa sababu za kujiuzulu katika chama hicho ikiwemo ukosefu wa mawasiliano bora, muongozo madhubiti wa chama na kupuuziliwa mbali kwa matakwa ya wakaazi wa Magarini kupitia chama hicho.

Mgombea wa nafasi ya ubunge wa Magarini kaunti ya Kilifi kwa chama cha DCP Furaha Chengo Kalama amejiuzulu kutoka chama hicho.

Hatua hii ni pigo kubwa kwa chama cha DCP katika eneo la Pwani baada ya mgombea mwengine wa eneo bunge la Banisa Adam Mohammed pia kujiuzulu kutoka chama hicho juma lililopita.

Uchaguzi huo mdogo wa Magarini umewavutia, viongozi mbalimbali wakiwemo Harrison Kombe wa ODM, Samuel Nzai wa Wiper, Furaha Chengo Kalama huku Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeahidi kuandaa uchaguzi huo Novemba 27 mwaka huu.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version