Sports

Harambee Stars Bado Ina nafasi ya kufuzu dimba la Dunia asema kocha Benni McCarthy

Published

on

Mkufunzi wa timu ya soka harambee stars Benni McCarthy anaamini bado kuna nafasi ya timu hiyo kufuzu dimba la dunia licha ya sare ya goli 1-1 dhidi ya Gambia Alhamisi uwanjani Stade Alessane Qatara nchini Ivory Coast.

Kwa mujibu wa mwalimu huyo akizungumza na wanahabari kabla ya kuivaa Gabon amesema bado kuna nafasi kubwa licha timu hiyo kuwa nyuma alama 7 baina yao na nambari moja Ivory coast.

“Sare dhidi ya Gambia haitusaidii wala haisaidi Gambia ila nachukua alama moja,pongezi kwa vijana kwa kuonyesha mchezo wa juu licha ya sisi kufanya mazoezi siku moja pekee.Tunakwenda kufanya marekebisho mazoezini kabla ya mechi dhidi ya Gabon Jumapili.”kocha Benni Mccarthy

Mwalimu huyo amefichua atafanya mabadiliko kwa kikosi cha kwanza baada ya wachezaji wa akiba kuonyesha makali yao wakiingia kipindi cha pili akitaja kinda Mohammed Bajaber,mshambulizi Jonah Ayunga na Williamson Lenkupae kwamba ni wachezaji ambao hawafai kuanza kitini.

“Ninajua kile kinachohitajika dhidi ya Gabon ukiangalia wachezaji walioanza walicheza vizuri mno,Lakini pia tukubali wachezaji nguvu mpya waligeuza ushirikiano uwanjani ni lazima tukubali ila wachezaji wote wana uwezo kutupa furaha dhidi ya Gabon ugani Nyayo.”

Vijana wa Nyumbani kwa sasa wanaketi nafasi ya nne kwenye jedwali la kundi F na alama sita baada ya mechi tano. Ivory coast wamekwea kileleni na alama 13 baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Burundi,Gabon ni ya pili na alama 12 nayo Burundi ikiwa ya tatu na alama 7 mkiani ni timu za Gambia alama 4 na Seychelles bila alama yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version