News

IEBC: Hatutaongeza muda wa usajili wa wapiga kura

Published

on

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imesema haitaongeza mda wa usajili wa wapiga kura kote nchini.

Makamishna wa Tume hiyo wameshikilia kwamba wakati muda huo uliyotengwa utakapokamilika, basi itakuwa ndio mwisho wa zoezi hilo.

Tume hiyo ilisema japo tayari imesajili zaidi ya wakenya milioni moja licha ya kukadiria kusajili idadi ya wakenya milioni 6.5, juhudi hizo zimeonekana kutofikia malengo hitajika.

IEBC ilikuwa imetangaza kusajili wapiga kura wapya milioni 6.5 ikilenga vijana wa Gen Z katika zoezi hilo huku vijana wenyewe wakizindua mpango wa NIKO KADI kama mbinu mbadala ya kusajili idadi kubwa zaidi ya wapiga kura kote nchini, bado juhudi hizo zimeokena kutofikia malengo ya IEBC.

Kamishna wa IEBC Hassan Noor Hassan aliwarai vijana wa kizazi cha Gen Z kutopuuza zoezi hilo na kutumia muda uliyosalia wa kipindi cha wiki moja kujisajili kama wapiga kura, akisema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wakenya wanapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao.

Noor alisema vifaa vya usajili wa wapiga kura vya kieletroniki ama KIEMS KIT vimewasilishwa hadi mashinani na maafisa wa Tume hiyo wanafanya kila juhudi kuhakikisha wakenya wanaojitokeza kwa usajili huo wanasajili.

“Tumepeleka vifaa vya kusajili wapiga kura wapya hadi mashinani vya KIEMS KIT, na tuko na matumaini makubwa kwamba tutafikia idadi tunayolenga ya wapiga kura wapya milioni 6.5, na tunawarai wakenya kujitokeza kwa wingi na kujisajili kwa kutumia muda uliyosalia wa wiki moja”, alisema Noor.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version