News

Jeremiah Kioni: Gachagua anafanyakazi kisiri na rais Ruto

Published

on

Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni amedai kuwa aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua anafanya kazi na rais William Ruto kisiri.

Kulingana na Kioni, Gachagua alikutana na viongozi katika kaunti ya Narok katika tarehe ambayo haijatajwa, ambapo alijaribu kueleza ni kwa nini chama cha DCP kilikuwa kinamnyima muaniaji wa wadi ya Narok mjini Joshua Ole Kaputa tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi mdogo ujao.

Kioni alidokeza kwamba mkutano huo ulikuwa na wanachama 15, miongoni mwao wakiwemo makasisi na kwamba kulikuwa na mpango uliowekwa kati yake na rais Ruto na Joshua angeteuliwa baadaye.

“Gachagua aliwaambia kuwa William Ruto tayari ametuma wajumbe kwao na walikuwa na mpango wa kuweka vyama vyao katika hali ya udhabiti kisha wakutane kujadiliana,” alidai Kioni.

Kioni hata hivyo alikana kufichua maelezo zaidi kuhusu mkutano huo wa siri, akisema “Alijieleza mwenyewe”.

Alishikilia kuwa chama cha Jubilee kiko tayari kufanya kazi na vyama vyenye nia moja na hakitashirikiana na yeyote anayehusika na mikataba mibaya ya kisiasa.

“Tungependa kufanya kazi na vyama vyenye nia moja ambavyo vinaamini katika kumbandua rais William madarakani “pata watu wako na mimi nipate wangu”, alibainisha Kioni.

Wakati huo huo aliwataka vijana kujiandikisha kuwa wapiga kura kwenye zoezi la usajili endelevu lililoanza rasmi Septemba 29, 2025

Taarifa ya Elizabeth Mwende

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version