News

KAA imemteua Moses Wekesa kuwa Mkurugenzi mkuu

Published

on

Bodi ya usimamizi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya (KAA) imemteua Moses Wekesa kuwa Mkurugenzi mkuu mpya.

Uamuzi huu umefuatia mchakato mkali na wa ushindani wa usaili uliomtambua Wekesa kama kiongozi bora wa kuendesha ajenda kabambe ya KAA.

Wekesa amesimamia miradi ya hali ya juu katika sekta mbalimbali za uchumi barani Ulaya, Asia, Pasifiki na Afrika.

Hapo awali, alihudumu kama mkurugenzi wa maendeleo ya Biashara katika shirika la KenGen, ambapo aliongoza ukuaji wa shughuli kuu za kampuni.

Aidha, bodi inatambua mpito bora wa uongozi, hasa wakati juhudi za kisasa za mamlaka ya KAA za kuboresha viwanja vya ndege zinaendelea kuimarishwa ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa.

KAA inaendelea kutekeleza mipango ya mageuzi, ikiwemo uboreshaji na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), unaolenga kuimarisha nafasi ya Kenya kama kitovu cha kikanda cha usafiri wa anga na usafirishaji wa mizigo.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version