News

Kadzeha: Wakaazi hawajahusishwa kwa miradi ya maendeleo

Published

on

Mwenyekiti wa kitaifa wa Taireni Association of Mijikenda, Peter Ponda Kadzeha amepinga madai kwamba wakaazi kuhusishwa katika miradi ya maendeleo katika eneo la Moi kadi ya Sabaki kaunti ndogo ya Magarini kaunti ya Kilifi kama kigezo hitajika katika utekelezaji wa miradi.

Akizungumza na Wanahabari, Ponda alisema kwamba hakuna vikao vyovyote vya umma vilivyofanyika kuwahusisha wakaazi wa eneo la Moi kabla ya kuanzishwa kwa mradi wa uchimbaji madini.

Ponda alipuuzia kauli za baadhi ya wakaazi wa eneo hilo ambao wanadai kuwa walishirikishwa kwenye kikao cha umma na kuhamasishwa kuhusiana na mradi huo wa uchimbaji madini.

“Kuna watu ambao wanatumia njia za mkato kwa kuwapa fedha wakaazi ili wakubali kuwa walishirikishwa kwenye mpango huo wa uchimbaji madini,” alieleza Ponda.

Aidha alisema kuwa harakati zao zinalenga kuhakikisha kuwa wakaazi wa Moi- Sabaki wananufaika kupitia raslimali hizo.

Taarifa ya Hamis Kombe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version