News

Kai, awalaumu mawaziri wa kaunti ya Mombasa kwa kuhujumu maendeleo

Published

on

Mwakilishi wa wadi ya Junda kaunti ya Mombasa Sylvester Kai amewakosa mawaziri katika serikali ya kaunti hiyo kwa madai ya kuhujumu maendeleo mashinani.

Kai alidai kwamba mawaziri hao wamedinda kushirikiana na wawakilishi wa wadi hali ambayo imechangia wakaazi wa kaunti hiyo ya Mombasa kukosa kutekelezewa miradi ya maendeleo.

Kai pia alidai kwamba baadhi ya mawaziri hao ni wafisadi na kuibua madai kuwa wanapania kuhakikisha baadhi ya wawakilishi wa wadi hawachaguliwi tena katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2027.

“Mawaziri wamepewa jukumu la kuhakikisha hakuna mwakilishi wa wadi ambaye atarudi 2027’’ alisema Kai.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version