News
Kalonzo:Rais Ruto ajiondoe mamlakani.
Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amemshauri rais William Ruto kuondoka madarakani pamoja na serikali yake ili kupisha mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa kitaifa.
Kalonzo alisema yanayoendelea nchini kwa sasa yamedhihirisha wazi namna idadi kubwa ya wakenya ambavyo hawaridhishwi na uongozi rais Ruto.
Kalonzo alidokeza kuwa taifa linaongozwa kwa misingi ya sheria na demokrasia, hivyo hakuna makosa kwa wakenya kuwakosoa viongozi walio madarakani vile vile kueleza hisia zao.
Kinara huyo alisema wito wa viongozi wa kanisa nchini wa kushinikiza mazungumzo ya kitaifa unafaa kuzingatiwa na kuhakikisha mazungumzo hayo yanahusisha pande zote husika.
Aliongeza kuwa kunaumuhimu wa serikali kusikiliza malalamishi ya vijana wa kizazi cha Gen Z, vile vile kuhakikisha maafisa wa usalama wanawapa Gen Z ulinzi wakutosha wakati wanapofanya maandamano mbali na kuwadhuru.
“Mambo ya Gen Z ni suala muhimu kabisa, lakini wakifanya maandamano ni lazima serikali ihakikishe ni maandamano ya amani, usije kupiga watoto risasi, unawauwa halafu unawalaumu, haifai”.alisema Kalonzo.
Taarifa ya Joseph Jira.