News

KDF kujigharamia chakula chao cha mchana.

Published

on

Wanajeshi nchini sasa watalazimika kujigharamia chakula chao cha mchana kuanzia Julai mosi mwezi ujao.

Hii ni baada ya serikali ya Rais William Ruto kusisitiza kuwa itafutilia mbali mpango wa ruzuku ya chakula kwa wanajeshi.

Hatua hiyo imezua taharuki miongoni mwa maafisa wa jeshi la ulinzi la Kenya yaani KDF hasa wale wa ngazi za chini wanaotegemea pakubwa mpango huo wa serikali.

Mpango huo wa chakula cha mchana uliokuwa ikifadhiliwa na hazina ya serikali kwa maafisa hao sasa utachulikwa na mfumo mpya wa lipa unapokula yaani “Pay as you Eat”.

Badhi ya maafisa wa vyeo chini walilalamika wakidai tayari wanabeba mzigo mzito wa kifedha kama vile mikopo huku wakisema wanahofu huenda wakalazimika kuwacha kula kabisa chini ya mpango huo mpya.

Kulingana na wizara ya ulinzi kufutilia mbali chakula hicho cha bila malipo ni njia ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuwapa wanajeshi uhuru wa kuchagua wanachokula.

Vile vile wizara hiyo inasema fedha zilizokuwa zikitumika kwa mfumo wa sasa zitatumika kuboresha miundombinu ya maeneo ya chakula, ununuzi wa vifaa vya upishi na kulipa madeni ya chakula yaliyosalia.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version