News

KeNHA: Ujenzi wa barabara ya Mombasa-Kilifi kukamilika Disemba 2026

Published

on

Mamlaka ya kitaifa ya kusimamia barabara kuu nchini KeNHA imesema ujenzi wa barabara kuu ya Mombasa-Kilifi inatarajiwa kukamilika kufikia mwezi Disemba mwaka ujao.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Luka Kimeli alisema kucheleweshwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya kipande cha kilomita 0-4 umechangiwa na uvamizi wa ardhi pamoja na ucheleweshaji wa fidia.

Kulingana na Mhandisi Kimeli, katika barabara hiyo hasa eneo la Bamburi Junction hadi Mtwapa inatarajiwa kufunguliwa mwezi Oktoba mwaka huu ili kuyawezesha magari kutumia barabara hiyo huku ujenzi wa madaraja mengine ukiendelea.

“Tumemaliza kujenga barabara ya kilimita 0-4 kutoka Bamburi Junction hadi Mtwapa na tutafungulia magari kutumia barabara hiyo mwezi Oktoba, tatizo ambalo lilikuwa linatuzuia kuendelea na ujenzi ni kucheleweshwa kulipwa fidia na uvamizi wa ardhi”, alisema Kimeli.

Wakati huo huo, maderava wahimizwa kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani hasa kwenye alama mpya zilizowekwa barabarani huku wananchi wakionywa dhidi ya uharibufu wa alama zilizowekwa barabarani kwani zengine zimegharimu pesa nyingi.

 Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version