Business
Kenya na Japan kushirikiana kibiashara na uchumi
Kenya inalenga kubadilisha uhusiano wake wa kiuchumi na Japan kutoka utegemezi wa misaada katika usawa wa kibiashara, mtaji na ubinafsi pamoja na ubunifu.
Rais William Ruto alihimiza serikali za ulaya kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa bidhaa za Kilimo za Kenya zinazouzwa nchini humo zikiwemo Parachici, Majani Chai na Maua.
Rais Ruto alitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka ili kufungua uwezo wa kiuchumi wa Afrika, akisema Afrika ni lazima itumie rasilimali zake kupitia biashara, uwekezaji na uvumbuzi.
Biashara kati ya mataifa hayo mawili ilikuwa kwa asilimia 35 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Hata hivyo biashara hiyo inatengemea zaidi Japan hali inayowazuia watengenezaji wa bidhaa humu nchini kushiriki kwenye biashara ya kimataifa ya bidhaa za viwango vya juu.
Ikumbukwe kwa mapato ya Kenya nchini Japan yamesalia kuwa ya kiwango cha chini ya dola ambacho ni dola milioni 70 ikilinganishwa na bidhaa za dola bilioni moja za Japani zilizoingizwa humu nchini.
Taarifa ya Pauline Mwango