Sports

Kenya yamaliza ya pili Duniani katika Riadha Mjini Tokyo,Japan

Published

on

Kenya imemaliza ya pili kwenye msimamo wa medali huku makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani yakikamilika Jumapili mjini Tokyo,Japan.

Kenya iliyokuwa ikiwakilishwa na wanariadha 58 imezoa jumla ya medali 11,dhahabu 7 fedha 2 na shaba 2.

Beatrice Chebet alinyakua dhahabu mbili (5000 na 10,000),Faith Kipyegon(1500m) Emmanuel Wanyonyi (800m)Faith Cherotich(3000msc) na Peres Jepchirchir (Marathon).

Washindi wa nishani za fedha walikuwa Faith Kipyegon mita 5000 na Dorcas Ewoi mita 3000 kuruka viunzi na maji  huku Edmund Serema akinyakua shaba ya mita 3000 kuruka viunzi na maji na Raynold Cheruiyot mita 1500.

Aidha Wakenya walivunja rekodi tatu za mashindano hayo wakiwa Emmanuel Wanyonyi,Faith Cherotich na Lilian Odira.

Marekani ilitwaa ubingwa kwa medali 16 za dhahabu fedha 5 na shaba 5.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version