Haya Ni kama marudio ya fainali ya mwaka 2012 uwanjani Allianz Arena, ambapo Chelsea walishinda kwa mikwaju ya penalti. Bayern haina muda wa kutulia baada ya msimu wa joto uliojaa mabadiliko makubwa, hasa safu ya ushambuliaji.
Washambuliaji Leroy Sane, Kingsley Coman, Thomas Mueller na Mathys Tel wote waliondoka majira ya joto. Ni wachezaji wawili pekee waliokuja: Luis Diaz kutoka Liverpool na Nicolas Jackson kutoka Chelsea kwa mkopo. Kwa kuwa Jamal Musiala na Alphonso Davies wako nje kwa majeraha ya muda mrefu, ukosefu wa usajili mpya ulichochea ukosoaji nadra kutoka kwa nyota wa timu, Harry Kane.
Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye si maarufu kwa kutoa kauli tata, alisema kikosi cha Bayern ni “chembamba”, akiongeza: “pengine ni miongoni mwa vikosi vidogo zaidi ambavyo nimewahi kuwa navyo katika maisha yangu ya soka.”
Akiwa na mabao manne na pasi mbili za mabao katika mechi tano za kwanza, Diaz ameanza kwa kasi nchini Ujerumani.
Lakini Chelsea, waliotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la Vilabu baada ya kuilaza Paris Saint-Germain miezi miwili tu iliyopita, huenda wakawa na mtihani mkubwa zaidi.
Kama Chelsea, Bayern wanatarajiwa kuvuka hatua ya makundi, lakini wanataka kufuzu moja kwa moja na kuepuka michezo ya mtoano ya nyongeza.
Mwaka jana, Bayern walimaliza nafasi ya 12 na walihangaika kumfunga Celtic, wakishinda kwa jumla ya 3-2.
Kane alikiri Jumamosi kwamba mzigo wa ziada uliwapunguzia kasi mwishoni mwa msimu: “Ni muhimu kuwa kwenye nane bora kwa sababu mchezo wa ziada unaweza kuleta tofauti kubwa. Mwaka jana, tulipocheza na Celtic nyumbani na ugenini wakati wa kipindi chetu cha kazi nyingi, kulikuwa na tofauti kubwa, na tukapoteza wachezaji wachache baada ya kipindi hicho cha Machi. Ni muhimu kuanza vizuri.”
Zaidi ya miaka 13 tangu Chelsea iwashinde Bayern katika uwanja wao wa nyumbani, timu zote mbili zimefanikiwa kutwaa taji jingine la Ligi ya Mabingwa.
Kuondoka kwa Mueller majira ya joto kumemwacha nahodha Manuel Neuer kama mchezaji pekee wa zamani kati ya timu zote mbili atakayecheza Jumatano.