News

Kindiki: Uchumi wa nchi umeimarika ikilinganishwa na miaka ya nyuma

Published

on

Naibu wa rais Prof. Kithure Kindiki amesema uchumi wa nchi umeimarika kwa sasa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Akizungumza katika eneo la Wundanyi kaunti ya Taita Taveta, katika ziara yake ya kuviwezesha vikundi mbalimbali pamoja na vyama vya ushirika wa akiba na mikopo ili kujiendeleza, Prof. Kindiki alisema mikakati ambayo imekuwa ikiwekwa kama ya uimarishaji wa sekta ya kilimo ilichangia kwa hilo kuafikiwa.

Aidha, Prof. Kindiki alisema uchumi wa Kenya ulikuwa umedorora zaidi wakati wa ujio wa uviko 19 ili kwa sasa uko thabiti.

Wakati huohuo, Prof. Kindiki alisema kilimo kimeimarika nchini kupitia ugavi wa mbolea ya bei nafuu ambayo imekuwa ikitolewa na serikali kuu kwa wakulima ili kuwe na utoshelevu wa chakula.

Naibu wa rais Prof. Kithure Kindiki na viongozi wengine katika kaunti ya Taita Taveta.

Vilevile, Prof. Kindiki alisema mpango wa ujenzi wa masoko ya kisasa umeanzishwa na wanapania kujenga masoko kwenye kaunti ya Taita Taveta.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version