News
KNCHR yatoa ripoti ya ukiukaji wa haki za kibinadamu nchini
Tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibindamu nchini KNCHR imesema zaidi ya watu 57 walipitia mateso na hata maafa katika hali tatanishi, mwaka huu wa 2025 pekee.
Tume hiyo ilitoa ripoti yake ya kila mwaka, ambapo ilibainisha kwamba mwaka huu pekee kumekuwa na visa 661 vya ukiukaji wa haki za binadamu.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Claris Ogangah alisema maafisa wa tume hiyo walibaini kwamba uchaguzi mdogo wa Novemba 27 haukuwa huru na haki na kwamba katika maeneo ya Kasipul uchaguzi huo ulishuhudia maafa ya watu wawili.
“Katika kipindi tulichoandaa ripoti hii, Tume imebaini kupokea jumla ya malalamishi 2,848. Miongozi ya malalamishi hayo ni poamoja na ukiukaji wa haki za kibinadamu”, alisema Ogangah.
Akisoma ripoti hiyo Kamishna wa Tume hiyo Prof Marion Mutugi amesema uchaguzi huo mdogo ulishuhudia pia uwizi wa kura, kwani maafisa wa Tume hiyo ambao walikuwa waangalizi wa uchaguzi walinyima nafasi ya kufuatilia uchaguzi huo.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi