News
KNUT yaahidi kushinikiza nyongeza ya asilimia 60 ya mshahara
Chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT kimeahidi kuishinikiza serikali kuongeza asilimia 60 ya mshahara kwa walimu pamoja na nyongeza ya asilimia 30 kama marupurufu.
Naibu Katibu mkuu wa KNUT Hesbon Otieno amesema mpango huo utajumuishwa katika mkataba wa makubaliano wa malipo CBA utaoanza mwezi Julia mosi nwaka huu.
Hesbon amesema walimu wanapitia changamoto nyingi katika kukidhi mahitaji yao kutokana na mpango wa serikali wa ushuru wa kila mara, akisema nyongeza hiyo ya mshahara itawapa motisha walimu katika utendakazi wao.
Wakati huo huo wadau mbalimbali wa masuala ya elimu nchini wameikosoa Tume ya kuajiri walimu nchini TSC kwa kushirikiana na serikali na kuondoa marupurupu ya walimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu.