News

KNUT, Yalalamikia Kucheleweshwa kwa Mgao wa Fedha Shuleni.

Published

on

Chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT tawi la Kilifi kimelalakimia serikali kuu kuhusu kuchelewa kusambaza mgao wa fedha wa kuendeleza shughuli za masomo.

Katibu wa chama hicho Johnathan Kenga amesema hali hiyo imekuwa ikitatiza utendakazi wa walimu shuleni licha ya kwamba pesa hizo hazifiki kwa wakati.

Akizungumza na Coco FM, Kenga amedokeza kwamba hali hiyo imechangiwa na mfumo wa usajili wa wanafunzi kupitia mfumo wa NEMIS ambao umekuwa ukihitilafiana na data ya wanafunzi inayofikia serikali kuu.

Katibu huyo vile vile amesema ana matumaini ya mabadiliko ya mfumo wa usajili wa wanafunzi kutoka NEMIS hadi KEMIS, akihoji kwamba huenda ukaleta mwanga katika sekta ya elimu nchini.

“Fedha zinachelewa sana na hata utendakazi wa zile shule kupitia kwa walimu wakuu inakuwa ngumu sana, kuna mambo mengi ambayo niyatimizwe yanahitaji fedha lakini bila fedha inakuwa sasa hakuna chochote kinaweza endelea, na licha ya kwamba inachelewa pia haitoshi. Kunadata ambayo huwa wanajaza walimu wakuu, inaitwa Nemis, Nemis huwa wanajaza enrollment ya kila shule, lakini kitu cha ajabu ni kwamba ile data inayotumwa kwa serikali sio ile inakuwa reflected kule kuonyesha kwamba hata ile capitation ambayo iko kwa kila mwanafunzi iko chini zaidi ya ule usajili wa shule”, alisema Kenga.

Wakati huo huo amependekeza kwa serikali itahakikisha inateuwa kiongozi mwenye tajiriba ya masuala ya elimu ili kushikilia uteuzi wa Afisa mkuu wa tume ya kuajiri walimu nchini TSC Nancy Macharia ambaye anatarajiwa kustaafu mwezi ujao. 

Kenga amesema iwapo suala hilo litatekelezwa basi madhila ambayo walimu wamekuwa wakipitia huenda yakapungua.

“Tungeomba wakati tunapopata yule mwengine atoke katika upande wa elimu, hata ikiwezekana pia katika hii miungano ya walimu kuna Kuppet kuna Knut, kama angetoka anayestahili ama anafikia vigezo kutoka kwa hii miungano miwili ingekuwa vizuri sana kwa sababu miungano inajua kabisa mahitaji na shida za walimu na elimu katika mashina”, aliongeza katibu Kenga. 

Na Joseph Jira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version