Sports

Kocha Domenico Tedesco Kocha mpya Fernabache ,Akichukua nafasi ya Jose Mourinho

Published

on

Kocha wa zamani wa Ubelgiji Domenico Tedesco amechukua nafasi ya Jose Mourinho kama meneja wa klabu ya Uturuki Fenerbahce kwa mkataba wa miaka miwili, klabu hiyo ya Istanbul ilitangaza Jumanne.

“Kocha wetu mpya ni Domenico Tedesco,” Fenerbahce walitangaza kupitia X, wakiongeza kuwa kocha huyo wa Kiitaliano-Kijerumani atasaidiwa na nahodha wa zamani wa timu hiyo Gokhan Gonul.

Tedesco, mwenye umri wa miaka 39, aliifundisha Ubelgiji kuanzia Februari 2023 hadi alipofutwa kazi Januari mwaka huu. Awali, aliwahi kuifundisha Schalke, Spartak Moscow na RB Leipzig.

Mreno Mourinho alifutwa kazi Agosti 29 baada ya klabu kushindwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikipoteza kwa Benfica kwenye mechi za mchujo.

Matarajio yalikuwa makubwa wakati kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 aliwasili Istanbul miezi 14 iliyopita.

“Hakuna ahadi. Lakini ni wazi kuwa lengo kuu, ndoto kuu ni kushinda Ligi Kuu ya Uturuki,” alisema kocha huyo aliyewahi kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili.

Hata hivyo, alishindwa kutimiza ndoto yake ya kumaliza ukame wa mataji uliyoikumba klabu hiyo bingwa mara 19 tangu mwaka 2014.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Real Madrid, Inter Milan, Manchester United, Tottenham Hotspur na Roma aliiongoza timu ya njano ya Istanbul kufika nafasi ya pili msimu uliopita nyuma ya Galatasaray.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version