Sports
Kocha Wa Bafana Bafana Ataja Kikosi Cha Mwisho Cha CHAN
AFRIKA KUSINI (SOUTH AFRICA)
Wanajiita Bafana Bafana kwa jina la Utani.
Afrika Kusini inaorodheshwa ya 56 msimamo wa kila mwezi wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA
Taifa hilo halijawahi kushinda taji la CHAN licha ya kushiriki mara tatu miaka ya (2011, 2014, 2025)
Kocha mkuu wa taifa hilo anaitwa Hugo Broos Hata hivyo katika majukumu ya CHAN amepewa kocha Molefi Ntseki ambaye ni mchezaji wa zamani wa taifa hilo na pia amewahi kuvinoa vikosi vya wachezaji wachanga timu ya taifa pamoja na vilabu vya Kaizer Chiefs na Bloemfontein.
Kocha huyo ametaja wachezaji 14 ambao hawana vilabu katika kikosi alichokitaja cha wachezaji 25
Badhi ya wachezaji nyota ni pamoja na Neo Maema anayepiga na Mamelodi Sundowns.
Bafana Bafana wako kundi C pamoja na Algeria,Guinea,Niger na Uganda.