News

Kongamano la 9 la ugatuzi laanza rasmi Homabay

Published

on

Wajumbe zaidi ya elfu 30 wanahudhuria Kongamano la 9 la Ugatuzi la mwaka wa 2025 katika kaunti ya Homabay linaloanza rasmi Agosti 12, 2025.

Akihutubia Wanahabari Gavana wa kaunti ya Homabay Gladys Wanga aliwahakikishia wajumbe watakaohudhuria kongamano hilo, kwamba usalama na mipango mingine muhimu imeimarishwa vilivyo.

Gavana Wanga alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni ujumuishaji, usawa na haki ya jamii, huku akisema kwamba masuala muhimu yanayohusu ugatuzi yatapewa kipau mbele katika kongamano hilo litakalofanyika katika shule ya upili ya wavulana ya Homabay.

Kauli yake iliungwa mkono na gavana wa kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti ambaye aliwarai wakenya kuunga mkono ugatuzi nchini, akisema umechangia maendeleo mengi mashinani.

Kongamano hilo la ugatuzi, pia linaadhimisha miaka 12 tangu serikali za ugatuzi kubuniwa nchini kupitia katiba mpya ya mwaka wa 2010.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version