Business
KPA :Bandari ya Lamu imevuna pakubwa
Bandari ya Lamu inazidi kujipatia umaarufu kama kitega uchumi kipya kwenye uchumi wa baharini kaunti ya Lamu lakini pia katika ukanda wa Afrika mashariki.
Meneja mkuu wa bandari hiyo, Abdulaziz Mzee aliema kwamba bandari hiyo imevutia idadi kubwa ya meli hali inayochochea uwekezaji mkubwa kama inavyokariri Mamlaka ya bandari nchini KPA.
Mzee alihoji kwamba katika wiki chache zijazo tayari meli 9 zinatarajiwa kutia nanga kwenye kaunti ya Lamu akiongeza kuwa tangia Januari mwaka huu jumla ya meli 13 zimepokelewa katika bandari hiyo
“Bandari hii inatarajiwa kuendelea kuleta faida katika uchumi wa baharini katika siku zijazo kutokana na uimarishaji wa uwekezaji ambao umekuwa ukifanyika tangu kuanzishwa kwa oparesheni za bandari eneo hili la Lamu” alisema mkurugenzi huyo mkuu wa bandari ya Lamu.
Taarifa ya Hamis Kombe