News

KUPPET yaitaka Tume ya TSC kuwaajiri walimu wanagenzi wa JSS

Published

on

Chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini, KUPPET, kimeitaka Tume ya huduma ya walimu nchini (TSC) kuwaajiri walimu wanagenzi hasa wale wa shule za sekondari za msingi (JSS).

Wakiongozwa na Katibu wa KUPPET tawi la Mombasa Lynet Kamadi, Viongozi wa Chama hicho walitishia kuandaa maandamano hadi katika ofisi za TSC endapo serikali haitatekeleza ombi hilo.

Akizungumza na Wanahabari, Kamadi alisema mfumo wa ajira za muda umekuwa ukiwalemea walimu kwani umewanyima uhakika wa kazi na kuathiri utulivu wao kazini.

Kwa upande wake, Carren Thuku na Bundi Kilemi walisema uhaba wa walimu shuleni umesababisha baadhi ya walimu kufundisha masomo ambayo hawana ufahamu nayo huku wakisema hawapaswi kubebeshwa mzigo wa kazi.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version