News

LSK tawi la Malindi yashtumu bunge la kaunti ya kilifi.

Published

on

Chama cha mawakili nchini LSK tawi la Malindi kimeshtumu ukiukaji wa sheria uliotekelezwa na viongozi wa bunge la kaunti ya kilifi kwa kupuuza agizo la mahakama la kusimamisha hoja ya kumbandua mamlakani spika wa bunge hilo Teddy Mwambire.

Mwenyekiti wa chama hicho Sirya Kiponda, alisema wawakilishi wadi katika bunge hilo walidhihirisha ukiukaji mkubwa wa katiba kinyume na jinsi walivyo ahidi kuilinda wakati walipochukua hatamu ya uongozi.

Kiponda aliitaja hatua ya viongozi hao kama ya kejeli kwa idara ya mahakama ambayo ni kati ya mihimili mikuu mitatu ya serikali inayofaa kushirikiana ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki.

“Serikali imetengenezwa na mihimili mitatu na endapo mkono mmoja unadharau utendakazi wa mkono mwengine inamaanisha serikali yote inashida na sisi kama wananchi tutapata shida katika maswala yetu wa kihaki kulingana na vile zinalindwa kwa katiba”, alisema Kiponda.

Kauli yake inajiri baada ya asilimia kubwa ya wawakilishi wadi wa bunge hilo kupiga kura ya kuunga mkono hoja ya kumbandua mamlakani Spika huyo licha ya agizo la hakimu Jesse Nyagah kuzuia kuendelea kwa mchakato wa kumuondoa Teddy Mwambire madarakani.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version