News
Madaktari kaunti ya Kwale kuanza mgomo wao rasmi.
Huduma za matibabu katika hospitali za umma kaunti ya Kwale zinatarajiwa kutatizika kuanzia juni 30, 2025 wakati madaktari watakapoanza mgomo wao rasmi.
Hii ni baada ya serikali ya kaunti hiyo kupuuza makataa ya siku 21 yaliyokamilika siku ya Jumapili 29 juni 2025, ya kushinikiza serikali hiyo kuangazia matakwa yao.
Katibu mkuu wa muungano wa madaktari KMPDU Daktari Ghalib Ali alisema moja ya suala kuu ambalo limeendelea kupuuzwa ni kupandishwa vyeo kwa madaktari hao ambao wamesalia kwenye nafasi moja kwa miaka kadhaa sasa.
Ghalib alisema wahudumu hao wamekuwa wakiongeza viwango vya masomo yao na hivyo wanafaa kupandishwa vyeo sawa na kulipwa marupurupu yao ya mishahara.
KMPDU vile vile ililaumu ofisi ya katibu wa kaunti ya Kwale na ofisi ya afisa mkuu wa afya kaunti hiyo kwa kupuuza muungano huo mara kwa mara.
Taarifa ya Joseph Jira