News

Mahakama ya Kilifi yaagiza kukamatwa kwa washukiwa wawili wa unajisi

Published

on

Mahakama ya Kilifi imetoa agizo la kukamatwa kwa Wanaume wawili walioshtakiwa kwa kosa la unajisi wa mtoto wa umri wa miaka 14.

Akitoa agizo hilo, Hakimu wa Mahakama hiyo James Mwaniki alimtaka Afisa anayechunguza kesi hiyo kushirikiana na Charo Changawa ambaye ni baba wa mlalamishi ili kuhakikisha washukiwa hao wanakamatwa.

Agizo hilo limetolewa baada ya washukiwa Kelvin Ngala na Emmanuel Kahindi waliokuwa wameachiliwa kwa dhamana kukosa kuhudhuria vikao vya Mahakama licha ya kufahamu wazi kwamba wana kesi ya kujibu.

Awali Mahakama ilielezwa kwamba washukiwa hao wakiwa wamejihami na kisu walimvamia mlalamishi akiwa njiani kuelekea nyumbani na kumsuma kwenye shamba la Mahindi kisha kumtishia kumua iwapo angepiga kelele huku wakimnajisi.

Wanaume hao walitekeleza kitendo hicho cha unyama mnamo tarehe moja mwezi Julai mwaka 2023 katika kijiji cha Maweni eneo la Takaungu kaunti ya Kilifi.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 25 mwezi huu. 

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version