News

Mahakama ya Kilifi yamhukumu mwanamme kifungo cha miaka 2 gerezani

Published

on

Mahakama ya Kilifi imemhukumu kifungo cha miaka miwili gerezani mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 36 kwa kosa la kumpiga bibi yake na kumsababishia majeraha.

Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama hiyo Ivy Wasike alisema kuwa mshtakiwa kwa jina Silas Shoka Mupe ana siku 14 kisheria za kukata rufaa iwapo hakuridhishwa na uamuzi huo.

Awali, kabla ya hukumu hiyo mahakama ilielezwa kwamba mnamo tarehe 8 mwezi septemba mwaka 2025, Mupe alimpiga na kumjeruhi bibi yake kwa jina Kadzo Karisa mwenye umri wa miaka 30.

Silas Shoka Mupe aliyehukumiwa kifungo cha miaka 2 gerezani katika mahakama ya Kilifi.

Mahakama hiyo pia ilielezwa kwamba Mupe ambaye ni mume wa bibi wanne na baba wa watoto 12, ana uzoefu wa kuwapiga bibi zake bila sababu za maana na kwamba hajukumiki katika mahitaji ya kimusingi ya watoto wake.

Wakati huo huo, mahakama hio ya Kilifi pia inatarajiwa kutoa uamuzi dhidi ya kesi za wanaume wawili walioshtakiwa kwa makosa ya unajisi: Joseph Kazungu na Elijah Murime.

Hakimu wa mahakama hiyo Ivy Wasike aliwaagiza washtakiwa Kazungu aliyeshtakiwa na kesi ya unajisi wa mtoto mwenye umri wa miaka 11 na Murime aliyeshtakiwa na kesi ya unajisi wa mtoto mwenye umri wa miaka 14, kuzuiliwa rumande hadi tarehe 1 mwezi Oktoba mwaka 2025 ambapo hukumu hiyo itatolewa.

Hakimu huyo aidha aliagiza wadhamini kwenye kesi hizo kurejeshewa udhamini wao, na washukiwa kurejeshwa tena mahakamani mnamo tarehe mosi mwezi Oktoba, 2025 ambapo uamuzi wa kesi hizo utatolewa.

Taarifa ya Teclar Yeri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version