News

Maiti tano zafukuliwa eneo la Kwa Binzaro kaunti ya Kilifi

Published

on

Maiti tano zimefukuliwa kutoka eneo la kwa Binzaro kaunti ya Kilifi, siku ya kwanza ya zoezi la kufukua maiti eneo hilo.

Maafisa wa upelelezi wanaohusika na mauaji kutoka idara ya DCI wamefukua makaburi 6 ambapo vipande 10 zaidi vya miili ya binadam viliepatikana.

Zoezi hilo la kufikua maiti lilifanywa kufuatia idhini ya idara ya mahakama huku maafisa wa upelelezi wakitarajiwa kuendelea kufukua makaburi 21 zaidi katika eneo hilo.

Mwanapatholojia wa serikali Daktari Richard Njoroge alitoa wito kwa wanafamilia ambao huenda walipoteza wapendwa wao kufika katika hospitali ya Malindi ambapo sampuli za DNA zitachukuliwa na kufanyiwa vipimo.

Naye afisa wa masuala ya dharura katika shirika la kutetea haki za binadam la Haki Afrika- Mathius Shipeta alidokeza kuwa safari hii miili ilikuwa imefichwa tofauti na ilivyoshuhudiwa katika msitu wa Shakahola.

Zoezi la ufukuaji maiti linatarajiwa kuendelea Ijumaa 22, Agosti 2025, huku  ikihofiwa huenda kuna watu zaidi walizikwa katika eneo hilo la Kwa Binzaro.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version