News
Makaburi 27 yagunduliwa Kwa Binzaro kaunti ya Kilifi
Shughuli ya kuyafukua makaburi eneo la Kwa Binzaro katika eneo la Chakama kaunti ya Kilifi imeanza rasmi siku ya Alhamisi Agosti 21, 2025.
Ufukuzi huo ulicheleweshwa kwa muda wa takaribani wiki mbili kusubiri kuwasili kwa maafisa wa kitengo cha kuchunguza mauaji kutoka kwa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai DCI baada ya Mahakama kutoa agizo la kuendelezwa kwa shughuli hiyo.
Awali maafisa wa kuchunguza mauaji kutoka kwa idara ya DCI walikuwa wametambua makaburi 27 ya watu ambao wanaaminika kuzikwa kutokana na itikadi potofu za kidini ambazo zinaendelezwa eneo hilo la Kwa Binzaro.
Kisa hicho cha Kwa Binzaro eneo ambalo liko karibu na Shakahola lilitambuliwa mwezi jana wa Julai mwaka huu wa 2025 baada ya kupatikana kwa mwili wa mtu msituni na mafuvu ambayo yanaaminika kuwa ya binadamu.
Taarifa ya Janet Mumbi