News

Mahakama ya Kilifi imerekodi kesi 90 za dhulma kwa watoto mwaka wa 2025

Published

on

Idara ya mahakama katika kaunti ya Kilifi imesema imerekodi kesi 90 za visa vya dhulma dhidi ya watoto mwaka wa 2025 pekee katika  huku kesi 46 zikiwa ni za wazazi kuwatelekeza watoto.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha mwezi wa haki kwa watoto, hakimu mkuu wa mahakama ya Kilifi Charles Obulutsa, amesema kesi za dhulma dhidi ya watoto zimekuwa zikitekelezwa na watu wa karibu wa muathiriwa hali ambayo inazidi kutia wasi wasi.

Hakimu Obulutsa amesema changamoto kuu ya kukabiliana na kesi hizo imekuwa ikitokana na ukosefu wa usahahidi kutoka idara mbali mbali hali ambayo imechangia waathiriwa wengi kukosa haki.

Wakati huo huo Obulutsa ameshinikiza mkuu wa sheria wa kaunti ya Kilifi kushinikiza mwakilishi wa kaunti upande wa idara ya afya kuhakikisha kunakuwa na urahisi wa kupatikana ushahidi wa daktari wakati wa kesi za dhulma dhidi ya watoto.

Kwa upande wake afisa wa idara ya watoto katika eneo bunge la Kilifi Kaskazini Apopo Waren ameshinikiza idara ya mahakama kuhakikisha inashughulikia kwa haraka kesi zote za watoto zilizo mahakamani ili kuhakikisha walioathirika wanapata Haki.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version