Sports

Manchester United Yamsajili Cunha

Published

on

Kilabu ya Manchester United imekamilisha usajili wa kiungo mshambulizi wa kilabu ya Wolves Matheus Cunha raia wa Brazil.

Kupitia kwenye tuvuti ya kilabu hiyo imetangaza kukubaliana na Wolves pamoja na matakwa ya kibinafsi ya mchezaji huyo

The Red Devils  wametumia kitita cha pauni milioni 62.5 kunasa mchezaji huyo mwneye umri wa miaka 26.

Mshambulizi huyo  atawasili kwa vipimo vya kimatibabu ugani Carringhton hapo kesho na tangazwa rasmi kuwa sajili wa kwanza kwa kocha mkuu Ruben Amorim.

Kwa mujibu wa nguli wa taarifa za Uhamisho Barani Ulaya Fabrizio Romano Cunha alitaka United pekee wala si kilabu yoyote ile licha kuvutia vilabu mbalimbali barani ulaya.

Mbrazil huyo anatarajiwa kutia wino mkataba wa miaka mitano uwanjani Old huku United wakiaminika sasa kuzamia kupata mshambuliz wakiwinda mshambulizi Victor Osimhen wa taifa la Nigeria na Victor Gyokeres wa taifa la Sweeden.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version