Sports
Mashemeji Derby: Gor kumenyana na Afc Raila Odinga Stadium
Mashemeji Derby
Kilabu ya Gor Mahia kuzindua uhasama na watani wao wa tangu jadi kilabu ya Afc Leopards katika debi la 97 leo uwanjani Raila Odinga Stadium mjini Homabay.
Mtanange huo ni kufa kupona kwa Kogalo ambao wana shinikizo za kupata alama zote tatu ili kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa wa ligi kuu Fkf Premier Ligi msimu huu.
Kwa Mujibu wa kocha mshikilizi wa Sirkali Zedekiah Zico Otieno mechi ya debi haina mwenyewe ila watacheza kwa ubora zaidi kupata ushindi.
“Kila mtu anajua debi huwa ngumu na haina mwenyewe,tunaenda kucheza kwa mfumo wa kushinda mechi hii na kupata alama tatu muhimu kwani ndio lengo letu kuu,Hata hivyo ni lazima mashabiki wawe tayari kwa matokeo yoyote kwani katika soka kuna kushinda,sare na kupoteza”.
Gor Mahia wanashikilia nafasi ya tatu kwenye jedwali la ligi kuu na alama 54 kutokana na mechi 31 huku Ingwe ikiwa ya sita na alama 46.