Sports

Mashindano Ya Shule Ya Upili Yaanza Kwa Kishindo Pwani

Published

on

Mabingwa watetezi wa soka kwa shule za upili eneo la Likoni Moi Forces Academy walianza vyema kampeni ya kutetea taji lao kwa kupata ushindi katika mechi zao zote za makundi.

Katika mechi ya kwanza waliitandika shule ya upili ya Likoni Boyz 2-0 kisha wakawageukia Timbwani na kuwatandika 4-0.

Katika mechi zingine kwenye kundi A, shule ya upili ya Mrima iliitandika Likoni Boys goli 1-0 huku Shikaadabu ikiigaragaza Tibwani magoli 2-0 na kwenye mechi ya pili Mrima ikapigwa magoli 3-1 na Shikaadabu.

Katika kundi B, shule ya upili ya Puma iliilambisha Mwahima magoli 2-1, huku Ushindi ikiilaza Al-Miraj magoli 3-0,nayo Bububu ikipata magoli 2-0 dhidi ya Al- Miraj na katika mechi ya pili Puma ikitoka sare ya 0-0 dhidi ya Ushindi nayo Bubububu ikicharazwa magoli 2-0 na Mwahima.

Katika upande wa akina dada, Kundi A, shule ya upili ya MFGA ilianza vyema kwa kujinyakulia magoli 7-0 dhidi ya Puma, kisha katika mechi ya pili ikaicharazwa na Mishi Mboko magoli 4-0, kisha Mishi Mboko ikailaza Shikaadabu magoli 3-0 na katika mechi ya pili Shikaadabu ikatoka 2-1 dhidi ya Puma.

Katika kundi B, Timwani ilitoka 1-0 dhidi ya Mtongwe Girls, na mechi ya pili Timbwani ikacharazwa 2-0 na Mwahima, nayo Ushindi ikatoka sare ya goli 1-1 na Mwahima, na kisha Mtongwe ikasawazisha mchezo kwa sare ya 0-0 dhihi ya Ushindi.

Kwenye  matokeo ya malindi sub county

Barani sec 3-0 Lango BAYA

Canon 0-1 Ganda sec

Barani 1-0 Ganda

Langobaya 2-2 Canon

Malindi 2-0 Bishop Kalu

Gede sec 0-4 Malindi High

Gede 2-0 Bishop Kalu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version