News

Mashirika ya kiserikali yaagizwa kutoa huduma kielektroniki.

Published

on

Mkuu wa utumishi wa umma nchini Felix Koskei, ameagiza mashirika yote ya serikali kuanza kutoa huduma za ununuzi kupitia mfumo wa kielektroniki wa serikali almaarufu e-GP mara moja.

Koskei alisema agizo hilo linafaa kutekelezwa kikamilifu bila kuchelewa, akisistiza kuwa ndiyo njia pekee ya kuhakikisha uwazi na kujenga imani ya umma.

Koskei alidokeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuepusha visa vya ufisadi ambao umewanyima wananchi fursa ya kunufaika na huduma za serikali.

Mkuu huyo wa utumishi wa umma pia aliwataka wasimamizi wa mashirika ya serikali kuzingatia uadilifu na nidhamu katika utekelezaji wa majukumu yao, na kuhakikisha mashirika hayo ya umma yanahudumu ipasavyo ili kufanikisha malengo ya serikali.

Aliyasema hayo kwenye mkutano uliowaleta pamoja makatibu wa wizara, wakuu wa mashirika ya serikali na asasi nyingine za usimamizi, ili kushughulikia masuala muhimu katika idara ya utumishi wa umma.

Taarifa ya Janet Mumbi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version