News
Mbadi atetea serikali kuhusu mfumo wa utoaji kandarasi
Waziri wa fedha nchini John Mbadi amepuuzilia mbali uamuzi wa bunge la kitaifa wa kusitisha agizo lake la kuwataka maafisa wote wa serikali kuu na kaunti kutumia mfumo mpya wa kieletroniki wa kutoa kandarasi- ‘EGP’.
Mbadi alisistiza kuwa bunge halina mamlaka ya kubatilisha amri ya serikali.
Waziri huyo alisema wanaopinga mfumo huo ni wale ambao mbinu zao za mkato za kupata kandarasi zimefungwa, na mfumo huo utatumika kudhibiti ufujaji wa fedha za umma.
Kauli hiyo iliungwa mkono na naibu rais Kithure Kindiki katika hafla ya kongamano la 13 la mshikamano wa kimaendeleo -DPF lililofanyika katika makao rasmi ya naibu rais.
Taarifa ya Joseph Jira