News

Mboko atoa wito kwa Wakenya kujiepusha na mambo maovu

Published

on

Mbunge wa Likoni kaunti ya Mombasa Mishi Mboko ametoa wito kwa Wakenya kujiepusha na mambo maovu pamoja na kauli ambazo huenda zikaichafulia jina taifa la Kenya kwani huenda zikaathiri sekta ya utalii.

Mboko ambaye alikuwa akizungumza katika kaunti ya Mombasa, alisema serikali inapaswa kuweka mikakati ifaayo ili kuimarisha sekta ya utalii kupitia uwekezaji.

Aidha, Mboko aliwahimiza Wakenya kudumisha uzalendo na pia kuwa katika mstari wa mbele kujenga taswira nzuri ya taifa la Kenya ili boresha utalii na pia kubuni nafasi za ajira kwa vijana nchini.

“Ni sekta ambayo lazima ipate fedha za kutosha na lazima tuweze kuiboresha sekta hii ili tupunguze ukosefu wa ajira kwa vijana’’ alisema Mboko.

Wakati huo huo, Mboko alisema mila na tamaduni za hapa nchini Kenya zinapaswa kutunzwa kwani ni mojawapo ya vivutio vya utalii.

“Hizi tamaduni zetu ni muhimu sana na lazima tuzidhibiti maana ni njia moja inayotupatia mapato na ni njia moja ya kuvutia mambo ya utalii katika taifa letu’’ aliongeza Mboko.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version